Mashabiki wa Yanga
Ligi Kuu

Yanga yafia Stand.

Sambaza kwa marafiki....

Klabu ya soka ya Yanga leo imekuona cha mtema kuni katika uwanja wa Kambarage jijini Shinyanga walipokuwa wanaikabili Stand united iliyokua nyumbani katika dimba lake la nyumbani.

Standa united wameweza kuula mfupa uliowashinda wengi baada kufanikiwa kuifunga Yanga kwa mara ya kwanza katika msimu huu wa Ligi Kuu Bara. Ikumbukwe Yanga ilikua haijapoteza hata mchezo mmoja tangu msimu uanze.

Alikua ni nahodha Jacob Massawe katika dakika ya 88 aliepeleka kilio jangwani baada ya kupokea krosi safi na salama kutoka kwa kiungo wa pembeni Mwinyi Elias na kujitwisha kichwa kilichomshinda mlinda mlango Klausi Kindoki. Mpaka mpira unamalizika Stand United 1 Yanga sc 0.

Kwa matokeo hayo yanaifanya Standa kua timu ya kwanza kuweza kuifunga Yanga msimu huu tangu uanze.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.