Luc Eymael, Kocha wa Yanga sc
Ligi Kuu

Yanga yamfukuza kocha wake!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga sc leo mapema hii asubuhi imeamua kuachana na kocha wake mkuu Mbelgiji Luc Aymael baada ya kumaliza Ligi Kuu Bara na mchezo dhidi ya Lipuli ya Iringa.

Barua rasmi kutoka katika idara ya habari ya Yanga imeainisha moja ya sababu ya kumfukuza kocha huyo ni pamoja na kauli ya udhalilishaji aliyoitoa jana baada ya mchezo dhidi ya Lipuli kumalizika.

Barua rasmi ya Yanga ikithibisha kumfukuza kazi Luc Aymael

Klabu ya soka ya Yanga imeonyesha kusikitishwa na kuomba radhi kutokana na vitendo hivyo vya kocha wao. Yanga imemaliza Ligi ikiwa nafasi ya pili nyuma ya Simba sc.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.