
Klabu ya soka ya Yanga imeendelea na usajili wake wa kimyakimya na mapema kama mwalim Mwinyi Zahera alivyosema huku wakifanikiwa kumsajili beki wa kati wa Simba.
Yanga imesaini Lamine Moro raia wa Ghana akitokea klabu ya Buildcom nchini Zambia kwa mkataba wa miaka miwili. Beki huyo mwenye miaka 25 huku akiwa na mwili mkubwa akimudu vizuri kucheza nafasi ya ulinzi.

Ikumbukwe Lamine Moro aliletwa nchini na klabu ya Simba kwa mara ya kwanza wakiwa na nia ya kumsajili. Moro alivaa jezi ya Simba katika michuano ya Sportpesa Supercup akifanyiwa majaribio na benchi la ufundi la Simba.
Kupitia mtandao wao wa kijamii Yanga wamethibitisha kumsajili Lamine Moro. Huku pia wakitarajiwa kuendelea kushusha majembe mengine.
Unaweza soma hizi pia..
Simba yatangaza rasmi kuachana na Morrison
Kumekuwepo na tetesi zinazomuhusisha Benard Morrison kurejea klabu yake ya zamani Yanga ambayo aliitumikia kabla ya kujiunga na Simba.
Simba: Tunawaza kumsajili Simon Msuva!
Kwasasa Simon Msuva yupo nchini akiwa hana klabu anayoichezea baada ya kushindwa kufikia muafaka na waajiri wake Wydad Casablanca
Kibwana: Inawauma lakini nipo Yanga!
Uwepo wa Kibwana Shomary tena kwa miaka miwili Yanga kunahatarisha nafasi za walinzi wa kushoto wa Yanga pia kina Yassin Mustapha na Bryson Raphael.
Nyota watakaompisha Ten Hag United wakiongozwa na Pogba
Pengine moja ya majina ya kushangaza zaidi ya wababe hao wa Uingereza wanasemekana kuwa tayari kuondoka katika klabu hiyo ni mhitimu wa akademi