Ligi Kuu

Yanga yamtimua kocha wake

Sambaza....

Uongozi wa klabu ya soka ya Yanga umethibitisha kuachana na aliyekua kocha wake Sebastian Nkoma aliyeiongoza Yanga Princess kwa muda mchache tu.

Sebastian Nkoma alijiunga na Yanga Princess baada ya Wanajangwani hao kuachana na kocha wake Edna Lema “Mourinhno”. Licha ya kujiunga na Yanga Princess December mwaka jana lakini leo taarifa rasmi ya klabu imethibitisha kuachana na kocha huyo mwenye uzoefu katika soka la wanawake.

“Uongozi wa Yanga unapenda kuutarifu umma umekubaliana kuvunja mkataba na kocha  mkuu wa wanawake. Yanga Princess, Sebastian Nkoma. Uamuzi huu umefikiwa kwa makubaliano ya pande zote mbili,” ilisema taarifa hiyo.

Kwasasa klabu ya Yanga itakua chini ya kocha msaidizi Fred Mbuna mpaka mwisho wa msimu. Mbuna ndio alikua na timu kama kocha msaidizi.

“Kwasasa bechi la ufundi la Yanga Princess litakua chini ya kocha Fred Mbuna mpaka msimu utakapomalizika,” ilisema taarifa hiyo

Mpaka sasa Yanga Princess inashika nafasi ya nne ikiwa na alama 22 katika michezo 12 waliyoshuka dimbani.


Sambaza....