Yikpe
Ligi Kuu

Yikpe hastahili kucheza hata daraja la pili

Sambaza....

Muhamasishaji mpya wa Yanga  Mheshimiwa Jerry Muro ambae ni mkuu wa wilaya ya Arumeru  leo ameongea na timu ya Wananchi Yanga kupitia redio ya Wasafi fm.

Katika mahojiano hayo Murro ameonekana kulalamikia ubora wa kikosi cha Yanga haswa wachezaji wa kigeni huku akiwatajaa baadhi yao kama Molinga na Yikpe.

Yikpe (Kushoto) akiwania mpira na Juma Nyosso

Jerry Murro” Huyu Yikpe tuongee ukweli hastahili hata kucheza Ligi daraja la pili, hana uwezo wa kucheza Yanga kabisa. Ukiangalia yeye ni mrefu sawa na John Bocco lakini hana vitu ambavyo Bocco anavyo, hana cha chenga wala kugeuka.

Ni afadhali ya Mrisho Ngassa, huyu “uncle” atatusaidia Yanga kuliko Yikpe hana msaada yoyote na Yanga.”

Sambaza....