TetesiUhamisho

Zidane aanza vita na Liverpool.

Sambaza....

Baada ya kukamilisha usajili wa Eder Militao, kocha wa Real Madrid,  Zinedine Zidane amehamisha nguvu zake na sasa anaitaka saini ya nyota wa Liverpool, Msenegali Sadio Mane.

Inaripotiwa kuwa,  zidane ana mipango ya dhati ya kukisuka kikosi cha Los Blancos kilichopoteza mataji kadhaa hadi sasa chini ya  wakufunzi Julen Lopetegui na Santiago Solari.

 Hadi sasa Madrid imeshayapoteza makombe ya klabu bingwa Ulaya na kombe la mfalme, na kwa sasa wako nyuma kwa alama 12  dhidi ya wapinzani wao Barcelonam katika msimamo wa ligi La liga.

Ubabe wa Madrid katika vita ya usajili huenda ukagonga mwamba hasa kwa Liverpool ambayo tayari inalisaka taji la ligi ya Uingereza na klabu bingwa ulaya, bila shaka hawatakubali Mane ajiunge na Los Blancos.

Mane ambaye tayari ameishaifungia Liverpool magoli 20 katika mechi 38 alizocheza, 7 kati ya magoli yote ameyafunga  mechi 4  hivi karibuni katika mechi  alizocheza katika mashindano yote.

Je unadhani ni rahisi kwa Madrid kumnasa Mane? Huku akiwa amesaliwa na mkataba wa miaka mine?


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.