Eliud Ambokile
Uhamisho

Ambokile huyoo Afrika Kusini!

Sambaza kwa marafiki....

Wachezaji wa Tanzania kwa sasa ni kama wanapishana tuu uwanja wa ndege kwenda nchi za watu kutafuta malisho mazuri na kucheza soka la kulipwa.

Sasa ni zamu ya Eliud Ambokile kupaa zake na kwenda nje ya nchi ili kujaribu bahati yake katika nchi ya Afrika Kusini. Taarifa rasmi iliyotolewa na Klabu ya Mbeya City inatnabaisha mpango mzima wa dili la Ambokile litakavyokua.

“Nyota wa klabu yetu pendwa Eliud Ambokile amejiunga rasmi na klabu ya Black Leopards F.C ya nchini Afrika Kusini kwa mkopo wa miezi mitatu.” Chanzo kilieleza.

Black Leopards F.C ni klabu imayoshiriki ligi kuu nchini Afrika kusini na ilianzishwa mwaka 1983 katika mji wa Venda uliopo kaskazini mwa Taifa hilo.

“Klabu yetu inamtakia heri na mafanikio katika utumishi wake mpya huko Afrika ya kusini.”

Kwa kujiunga na klabu hiyo sasa Ambokile anakwenda kuungana na mlinzi wa zamani wa Simba na Taifa Stars Abdi Banda.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.