Tetesi

Auseems kutambulishwa Yanga

Sambaza....

Aliekua kocha wa Klabu ya Simba sc Patrick Auseems huenda wakati wowote akahamia upande wa pili wa mitaa ya Twiga na Jangwani na kuhudumu kama kocha mkuu.

Auseems amehudumu msimu mmoja na nusu katika klabu ya Simba na kuwapa taji la Ligi Kuu Bara na kuwafikisha robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Mbelgiji huyo alitimuliwa katikati ya msimu wa 2019/2020 baada ya maboss wa Msimbazi kutofautiana nae.

Yanga baada ya kumfukuza Luc Aymael kutokana na sababu za utovu wa nidhamu na kutoa maneno ya ubaguzi wapo sokoni kutafuta kocha mpya. Baadhi ya majina yamekua yakihusishwa kwenda kujiunga na Yanga kama Ettiene Ndayiragije, Meky Mexime na Hitimana Thiery.

Kile kishindo alichotangaza msemaji wa Yanga Antonio Nuggas huenda ndio kanakaribia kutimia. Tuendelee kuweka bando tuu na kuendelea kufuatilia tovuti ya Kandanda kwa habari zaidi za usajili.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.