Djuma katika majukumu yake akiwa na Klabu ya Simba
Ligi Kuu

Aussems: Jana nimekunywa kahawa na Masoud, kabaki Dar kuwafuatilia Yanga.

Sambaza....

Kocha Mkuu wa kikosi cha wekundu wa Msimbazi, Simba Sports Club, Mbeligiji, Patrick Aussems amesema hana noma lolote na kocha msaidizi Masoud Djuma kama ambavyo watu wamekuwa wakidukuadukua taarifa hizo.

Akizungumza na mtandao huu mara tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa Jijini Mwanza Aussems amesema hata jioni ya jana walikaa pamoja na kunywa kahawa na kupanga kwa pamoja namna wanavyoweza kuifunga Yanga katika mchezo wa ligi Septemba 30 mwaka huu.

Aussems ameyasema hayo baada ya kuulizwa mara kadhaa kuhusu kutokuwapo kwa Masoud kwenye msafara uliofika hapa jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa ligi siku ya Alhamis dhidi ya Mbao FC kwenye uwanja wa CCM Kirumba.

Amesema amemuacha Masoud Djuma jijini Dar es Salaam kama ilivyokuwa kwenye safari ya Mtwara kwa sababu amemuomba aendelee kufuatilia kwa umakini michezo ya Yanga pamoja na kuendelea na Programu ya mazoezi na wachezaji waliochelewa kuripoti kama Jjuuko Murushid na Haruna Niyonzima.

“Hawa wachezaji wanatakiwa kujiandaa, kwa hiyo walitakiwa kubaki Dar na kujifua na kuwa fit kama wachezaji wengine lakini pia nimemuomba Masoud kuendelea kuwaangalia Yanga, kwani tutacheza nao ndani ya siku 10 zijazo kwa hiyo tunahitaji kuwajua, unajua mimi na Masoud tumekunywa Kahama jana jioni tu,” Aussems amesema.

Simba imewasili jijini Mwanza ikiwa na wachezaji 21, huku wachezaji Hassan Dilunga, Mzamiru Yassin na Asante Kwasi wakiachwa kutokana na kuwa na majeraha.

Wachezaji waliofika jijini Mwanza ni pamoja na.


  1. Aishi Manula
  2. Deo Munishi
  3. Nicholas Gyan
  4. Shomari Kapombe
  5. Paul Bukaba
  6. Pascal Wawa
  7. Erasto Nyoni
  8. Yusuph Mlipili
  9. Jonas Mkude
  10. Mohammed Ibrahim
  11. Adam Salamba
  12. Emmanuel Okwi
  13. John Boko
  14. Meddie Kagere
  15. Clatous Chama
  16. Mohammed Hussein
  17. Mohammed Rashid
  18. Said Ndemla
  19. Shiza Ramadhan Kichuya

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x