John Bocco
Ligi Kuu

Baada ya kuia Yanga Bocco apewa zawadi yake na TFF!

Sambaza....

Nahodha wa Simba sc Papaa John Raphael Bocco baada ya furaha ya kuifunga Yanga katika mchezo wa nusu fainali ya FA TFF ni kama wameendelea kumnogeshea sherehe hiyo baada ya kuangazwa kama mshindi wa mwezi June.

Bocco amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi June baada ya kuwapiku Atupele Green wa Biashara Utd na Martine Kiggi wa Alliance school fc aliokua anagombea nao tuzi kwa mwezi wa sita.

Bocco

John Bocco amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo minne aliyocheza na kufanikiwa kuipa ubingwa klabu yake ya Simba kwa goli lake katika mchezo dhidi ya Mbeya city na mawili dhidi ya Mwadui fc.

Kwa upande wa tuzo ya kocha bora wa mwezi imekwenda kwa kwa kocha wa Alliance fc Kessy Mzirai. Katika mwezi June Alliance imefanikiwa kupata alama 7 katika michezo mitatu waliyocheza. Walifanikiwa kumfunga Mbeya city, wakapata sare dhidi ya Polisi Tanzania na kumfunga Coastal Union.

Kessy ametwaa tuzo hiyo ya kocha bora baada ya kuwazidi washindani wake Sven wa Simba na Luc Aymael wa Yanga.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.