Sambaza....

Beki kisiki na wakutumainiwa aliekua amekaa nje mdaa mrefu kwasababu ya majeruhi anakaribia kurudi uwanjani. 

Beki Salim Mbonde aliekua ameumia goti kwa muda mrefu tangu msimu uliopita sasa amepata nafuu na kuanza mazoezi mepesi na wenzake katika uwanja wa Bokko beach veteran. 

Manara alipokua akiongea na waandishi wa habari, alithibitisha kuwa mchezaji wao huyo ameanza mazoezi mepesi.

“Wachezaji wetu wawili majeruhi Shomari Kapombe na Salim Mbonde pekee ndio majeruhi, Salim Mbonde ameanza mazoezi mepesi na wenzake wakati wowote atakua tayari kutumika katika michezo ya raundi ya pili” 

Salim Mbonde tangu ajiunge na Simba akitokea Mtibwa Sugar amekuwa majeruhi ambayo yanmfanya kushindwa kuitumikia ipasavyo klabu yake mpya. 

Kurudi kwa Salim Mbonde kunamaanisha kuzidi kuongezeka kwa ushindani katika eneo la beki wa kati, mpaka sasa nafasi hiyo ina mabeki watano lakini mwalimu Patrick amekua akiwatumia Pascal Wawa na Erasto Nyoni sana, huku Juuko Mursheed akipata nafasi mara chache Yusuph Mlipili na Paul Bukaba wamekua na nafasi finyu katika kikosi hicho.


Sambaza....