Yikpe
Uhamisho

Bila milioni 20 siondoki Yanga-YIKPE

Sambaza....

Yanga kwa sasa inahangaika na sakata la Bernard Morrison kwa kiasi kikubwa baada ya kusemekana amesajili katika klabu ya Simba wakati ana mkataba na Yanga.

Wakati Yanga inahangaika na suala hili kuna habari kuwa mshambuliaji wa Yanga kutoka Ivory Coast, Gislain Yikpe amedai kuwa hawezi kuvunja mkataba na Yanga mpaka alipwe milioni 20.

Mshambuliaji huyo ambaye asilimia kubwa ya mashabiki hawamkubali kutokana na kiwango chake kuwa hafifu amesisitiza kwake ni ngumu kuondika Yanga kama hajalipwa kiasi hicho cha Pesa.

“Kama Yanga inataka kuvunja mkataba wangu wanatakiwa kunilipa Dola 9000 (Zaidi Ya Milion Ishirini Za Kitanzania) na mshahara wa miezi mitatu”. Alisema Gislan Yikpe mshambuliaji wa Yanga.

Mpaka sasa hivi Yikpe ana mkataba na Yanga ambao unamfanya kuwa ni mchezaji halali  wa Yanga kitendo ambacho mashabiki wengi wa Yanga hawataki kukisikia.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.