Sambaza....

Baada ya kuvunja mkataba wake na klabu ya Yanga kutokana na kutokuitumikia kwa muda mrefu mshambuliaji Mzimbabwe Donald Ngoma ni rasmi sasa amejiunga na klabu ya Azam fc kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Tovuti hii mwanzo iliandika tetesi za mshambuliaji huyo kujiunga na Wanalambalamba hao lakini sasa ni rasmi amesajiliwa na timu hiyo.

Chanzo cha kutoka Azam kimesema ” Uongozi wa klabu bingwa ya Africa Mashariki na Kati, Azam unapenda kuthibitisha kuwa imeingia makubaliano ya usajili na mshambuliaji Donald Ngoma, kwa ajili ya msimu ujao 2018/2019.”

Baada ya kuingia makubaliano hayo muda wowote kuanzia sasa AzamFc inatarajia kumpeleka África Kusini katika hospitali ya Vincent Pallotti jijini Cape Town, kwaajili ya kumfanya vipimo vya afya ili kuona ni kwa kiasi gani majeraha yaliyokuwa yakimsumbua yamepona.

Klabu hiyo inategemea kumtumia mapema katika michuano ya Kagame mapema mwezi ujao. Donald Ngoma anakwenda kuungana na kina Mbaraka Yusuph, Yahya Zaid na Mbaraka Yusuph kutengeneza safu ya ushambuliaji ya Azam.

Sambaza....