Said Hamis Ndemla.
Ligi Kuu

“First eleven” inayokaa benchi VPL!

Sambaza....

Ligi Kuu Bara mpaka sasa imefika katika raundi ya 24 huku ikisimama kupisha michuano ya Azam Sports Federation Cup kwa wiki hii. Vita ni kali na ushindani ni wa hali ya juu haswa katika eneo la kushuka daraja.

Tovuti ya Kandanda inakuletea baadhi ya wachezaji ambao wamekosa ama wamepoteza nafasi katika vikosi vya kwanza vya timu zao kwa sababu mbalimbali ikiwemo majeruhi ama kushukwa kwa uwezo, huku wengine walikua wachezaji muhimu katika klabu na timu ya Taifa.

1. Said Mohamed “Nduda”- Mtibwa Sugar.

Kipa wa zamani wa Simba, Yanga na timu ya Taifa lakini pia aliwahi kua kipa bora katika michuano ya COSAFA. Ameshindwa kabisa kufua dafu mbele ya mkongwe mwingine Shabani Kado katika lango la Mtibwa Sugar.

2. Paul Godfrey “Boxer”- Yanga.

Msimu uliopita alikua sehemu muhimu ya kikosi cha Mwinyi Zahera na kupelekea kujumuishwa katika kikosi cha Taifa Stars na mwalimu Ettiene lakini majeruhi yamemrudisha benchi na kumfanya kukaa kumwangalia kaka yake Juma Abdul akitumikia nafasi ya mlinzi wa kulia katika kikosi cha Yanga.

Gadiel Michael akikitumikia kikosi cha Taifa Stars

3. Gadiel Michael Mbaga- Simba.

Akitoka kuwa mchezaji muhimu katika vikosi vya Yanga na Stars Gadiel amejikuta akipoteza nafasi mbele ya Tshabalala na hivyo kua msindikizaji tuu katika kikosi cha Simba na haswa alipokuja kocha mpya Sven Vandebroek.

4. Kenedy Kipepe- Coastal Union.

Akiwa kwenye kiwango kizuri lakini ameshindwa kupenya katika kikosi cha kwanza mbele ya Ibrahim Ame na Bakari Mwamunyeto na hivyo kujikuta akisugua benchi tofauti na alivyokua mchezaji muhimu katika kikosi cha Wanalizombe Majimaji fc.

5. Yusuph Mlipili- Simba sc.

Beki wa kati aliekaa Simba msimu wa tatu sasa amekua akiwaangalia wakongwe Pascal Wawa na Erasto Nyoni wakicheza. Kwa msimu huu ameshindwa kabisa kucheza hata mchezo mmoja wa Ligi huku pia akikosa hata nafasi ya kukaa katika benchi la Simba akizidiwa na Kenedy Juma pia.

Kiungo wa Namungo fc John Mbisse!

6. John Mbise- Namungo fc.

Alianza vizuri katika kikosi cha Namungo katika michezo ya mwanzo huku akiwa na muunganiko mzuri na Mo Ibrahim lakini baada ya kupata majeruhi ya enka yakamrudisha nyuma na hivyo kupoteza nafasi mbele ya viungo wengine wa Namungo.

7.  Salum Kihimbwa- Mtibwa Sugar.

Akiwa ametoka kucheza vizuri katika michuano ya Mapinduzi kiungo huyo fundi wa pembeni alijikuta akikosa tena nafasi ya kuitumikia Mtibwa huku majeruhi pia yakichangia, Mwalim Katwila amekua akiwatumia Mhesa, Frank au Awadh Salum katika eneo lake.

8. Said Ndemla “Daktari”- Simba.

Ndemla amejikuta akiwa mchezaji wa kukaa jukwaani baada ya kushindwa kabisa kumshawishi mwalimu Sven Vandebroek. Ndemla amejikuta akipoteza nafasi mbele ya Cleotus Chama na Sharaff Shiboub licha ya mwalimu msaidizi Selemani Matola kukiri juu ya uwezo wake.

Patrick Sibomana “PS Machine”

9. Richard Djodi- Azam fc

Alianza vizuri katika michezo ya mwanzo lakini baadae akawa mchezaji wa kuingia na kutoka katika kikosi cha Azam fc. Azam fc ni moja pia ya klabu yenye washambuliaji wengi katika kikosi chake ikiwa na washambuliaji kama Obrey Chirwa, Donald Ngoma, Shabani Chilunda na Andrew Simchimba.

10. Frank Ikobella- Kagera Sugar.

Ikobella akitokea Mbeya city alianza na moto wa mabao huku akiibuka mchezaji muhimu katika kikosi cha Mexime akicheza pacha na Nasorro Kapama. Lakini majeruhi yamemfanya kukosekana tena mpaka mwisho wa msimu.

11. Patrick Sibomana- Yanga.

Mwanzoni alionekana kama mkombozi katika safu ya ushambuliaji ya Yanga haswa katika kupiga mipira iliyokufa, lakini dirisha dogo limebadili kabisa maisha yake ndani ya timu baada ya ujio wa Ditram Nchimbi na Benard Morisson.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.