Gerson Fraga Vieira
Stori

Fraga ni kipimo halisi cha umakini wa Simba ya Senzo!

Sambaza....

“Bongo bwana wakikukataa wamekukataa, hakuna namna utafanya wakukubali tena.” Hayo ni maneno ya rafiki yangu mmoja katika stori zetu za soka kumhusu Kiungo wa Simba Gerson Fraga.

Imekua kasumba kubwa kwa timu nyingi za Tanzania kuendeshwa kwa mihemko ya watu hususani vilabu vya Simba na Yanga. Tabia iliyo mbaya zaidi, inaua mpira, ikatae kabisa sio nzuri.

Yaani iko hivi, mashabiki wakimshabikia sana mchezaji wa pande A lazima pande B watamtaka, na wakimkataa au kutomkubali flani basi na uongozi utazama huko huko, hii ni fedheha.

Gerson Fraga akisaini kuitumikia Simba mbele ya Hanse Pope.

Mpira ni mchezo wa ufundi, unahitaji akili kubwa kuuelewa mchezo na wachezaji, ukiweka ushabiki hakuna utakachoweza zaidi ya mawazo na kushindwa tu.

Ni wajuzi wa mpira tu watakao kuambia kuwa Mbrazil Gerson Fraga ni Mchezaji mkubwa sana kunako klabu ya Simba. Mashabiki waliowengi wanaupepo wa watu, hawajamkubali sana huyu mtu bali wamembeza kuliko kumkubali haya ni mazoea.

Maswali ni mengi juu yao, Kwanini hawajamkubali? Au kwa kua anacheza eneo moja na kipenzi chao Mkude?, ama kwavile hana kiduku kichwani? Ni mengi ya kujiuliza lakini ukweli ni kwamba Fraga ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa sana wa kucheza mpira.

Gersona Fraga “Mkata Umeme”

Simba na CEO wake Senzo wanayo kazi ya kujibu kwa wajuzi siku wakimuacha kiumbe huyu nahodha wa timu ya vijana Brazil, mwaka 2009 nahodha wa Neymar na wakali wengine kibao.

Akili yake uwanjani ni kubwa mno, inatoa maelekezo kwa miguu, kichwa, kifua na kiwiliwili vyote vinatii na kutenda. Hachagui kiwanja, iwe Liti Singida ama Chamazi complex, yeye ananesa tu, mtata mmoja mbrazil mwenye roho ya Buza.

Ukimpa dimba la kati chini (Defensive midfielder), utasema umesimika kibao cha “Hakuna Njia” uwanjani, hapiti mtu na safari nyingi za timu pinzani huishia kwake.  Jamaa anaanzisha mashambulizi na kumudu ulinzi, kiujumla ni kiungo mkabaji mwenye sifa zote chanya.

Gerson Fraga akimthibiti Bruce Kangwa wa Azam fc

Simba walimuacha okwi, James kotei Chuma, kipenzi cha Mashabiki, leo baadhi yao wanajutia uamuzi ule, kwanini kesho waruhusu Fraga aondoke? (Ulizo)

Kama nia ni kuijenga timu ya kiushindani basi haina haja ya kuishi kwa mihemko bali kwa mipango madhubuti, huu ndio wakati wa kutenganisha dhahabu na mchanga.

Haina haja ya kumuacha Fraga ilihali unamtegemea Jonas Mkude pekee, Senzo na Simba kwa ujumla kupitia kamati ya Ufundi wapigieni simu waambieni Mwandishi wa Kushoto Nimesema Fraga ni Mchezaji Anayepaswa Kubaki Msimbazi.

Sambaza....