Uhamisho

Huyu hapa kocha mpya wa Yanga

Sambaza....

Klabu ya soka ya Yanga baada ya kuachana na Cedrik Kaze raia wa Burundi kutokana na matatizo ya Kifamilia leo hii imemtangaza kocha mpya watakaekua naya msimu ujao wa Ligi.

Yanga imemtangaza Zlatiko  Klempotic raia wa Serbia kua kocha wao mpya ambapo atakwenda kusaidiana na Juma Mwambusi kama kocha msaidizi.

Zlatiko alikua kocha wa Polokwane City ya Afrika Kusini kabla ya kuamua kuvunja mkataba na kujiunga na Yanga. Ni kocha mwenye uzoefu na soka la Afrika.

Amepitia vilabu vinne vya Afrika TP Mazembe, Zesco, Rayol Sports na Polokwane alipokua mpaka sasa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.