Uhamisho

Kaseke ndio basi tena Yanga!

Sambaza....

Kiungo wa zamani wa Mbeya City na Singida United Deus  amezungumzia hatma yake katika klabu ya Yanga baada ya kuibuka tetesi kua huenda akatemwa na miamba ya soka ya Jangwani Yanga Sc.

Baada ya GSM kuweka mkono katika usajili wa Yanga na kuweka wazi wanataka kusajili wachezaji wenye hadhi ya Yanga na kuifanya Yanga ya Kimataifa zaidi. Kutokana na usajili huo wa nguvu unaoelekea kufanywa Yanga kumehatarisha nafasi ya Deus Kaseke kuendendelea kusalia Jangwani.

Deus Kaseke.

Baada ya sintofahamu hiyo Kaseke hakusita kuweka wazi hatma yake ya msimu ujao.

Kaseke “Nipo tayari kuondoka Yanga hiyo naweka tiki ikitokea timu itakayokuja na maslahi mazuri ninaweza Yanga.

Hakuna mchezaji anaetaka kucheza hapa nchini kwa muda wote, ikitokea nafasi ya kwenda nje sawa lakini pia hata hapa ndani pia naweza kuondoka endapo timu itakubaliana na Yanga na mimi pia maslahi yangu.”

Deus Kaseke amezungumza hayo katika mahojiano ya kipindi cha Wasafi fm.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.