Ligi Kuu

Kaze: Kesho ni mechi “special”.

Sambaza....

Kuelekea mchezo wa kesho wa “Derby” kati ya Simba na kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze amseme kesho ni siku special na hakusita kitanabaisha malengo yao ya msimu huu. Kaze ameyasema hayo mbele ya waandishi wa habari leo kuelekea mchezo wa kesho.

“Naona ni mchezo special na ndio maana hata maandalizi yamekua special hapa unaona hata hii “press conference” imekua special pia.” Cedrik Kaze kocha wa Yanga.

Kocha msaidizi wa Yanga Cedric Kaze (katikati), Deus Kaseke (kulia) na Karim Boimanda Afisa habari wa bodi ya Ligi(kushoto)

Kocha wa Yanga pia amekiri kucheza na Simba ambayo ni bora na kuheshimu mashindano waliyotoka katika michuano ya CAF, na pia Kaze amesema hawatafuti kutokupoteza mchezo bali wanapambania malengo yao.

“Tunakwenda kucheza na timu iliyo bora ambayo imetolewa katika michuano ya Afrika, timu yenye wachezaji wakubwa Afrika na wenye uzoefu mkubwa.

Kikosi cha Simba kilichotolewa katika robo fainali ya kombe la shirikisho Afrika.

Sisi kwetu tunataka alama tatu ambazo ni muhimu kuelekea kutwaa ubingwa wetu.
Kesho tunaenda kutafuta point 3 hatuendi kutafuta “unbeaten”. Tunakwenda kulinda malengo yetu tuliyojiwekea tangu mwanzo wa msimu.” Cedric Kaze

Yanga itawakosa wachezaji wawili pekee kuelekea mchezo wa kesho huku Djuma Shaban akirudi mazoezini.

“Tutamkosa Yocouba Sogne na Chico Ushindi ambae alipata matatizo na kupelekwa hospitali.
Lakini wachezaji wengine wapo vizuri hata Djuma Shabani amerejea mazoezini.” Alimalizia kocha msaidizi wa Yanga.


Sambaza....