Kikosi cha Simba kikiwa mazoezini.
Uhamisho

Kipa wa Simba amwaga wino Lipuli.

Sambaza....

Mlinda mlango mzoefu aliepitia vilabu kadhaa vya Ligi Kuu Bara Deogratius Munishi “Dida” amerejea tena katika ligi baada ya kukubali kusaini kandarasi fupi ya miezi sita.

Deo Munishi mara ya mwisho kuonekana Ligi Luu Bara alikua anawatumikia Wekundu wa Msimbazi Simba sc sasa amerudi akiwa na Wanalaluhengo Lipuli fc.

Dida kipa wa zamani wa Simba, Yanga na Azam fc amesaini kandarasi ya miezi sita ili kuweza kuitumikia Lipuli fc  yenye maskani yake jijini Iringa.

Deo Dida pia alionekana akiwa na timu ya Taifa ya Beach Soccer hivyo kuonekana bado yuko fiti kuweza kutumika katika Ligi Kuu Bara. Lipuli fc pia imemsajili kwa mkopo wa miezi sita beki David Mwantika kutoka Azam fc.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.