Tetesi

Kiungo akanusha kusaini Yanga!

Sambaza....

Kiungo wa Alliance Fc David Richard Ulomi amekanusha tetesi za yeye kusaini Yanga na kusema hakuna kitu kama hicho huku pia akiweka wazi yeye ni mchezaji huru baada ya kumalizana na Alliance fc.

David Richard “Nasikia kwa watu tu lakini mimi sijasaini popote wala sijazungumza na Yanga mpaka sasa. Mkataba wangu na Alliance umekwisha nikweli kwasasa ni mchezaji huru”

Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji saba wa msimu uliopita waliofunga Hatrick amesema yupo tayari kwenda klabu yoyote kikubwa ni mzigo tu wa maana ndio utakaoamua wapi atakwenda msimu ujao.
“Kikubwa ni maslahi tu sina pingamizi na kusaini Yanga au klabu nyingine yoyote. Muhimu ni kuelewana na kuweza kufanya kazi popote tu.” Alimalizia David mwenye mabao nane kwenye Ligi Kuu Bara


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.