"Walianza kunifwatilia muda tuu kumbe hata kabla ya kusaini Dodoma Jiji, waliniona na wakaomba video zangu wakatumiwa mechi nilizocheza na kocha akapendekeza jina langu kusajiliwa katika timu yake.
Kiungo huyo ni miongoni mwa wachezaji saba wa msimu uliopita waliofunga Hatrick amesema yupo tayari kwenda klabu yoyote kikubwa ni mzigo tu wa maana ndio utakaoamua wapi atakwenda msimu ujao.