Sven Vandebroek na Selemani Matola
Ligi Kuu

Kocha Simba afichua jinsi watakavyobeba ubingwa kesho!

Sambaza....

Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck ameweka hadharani mbinu atakazotumia katika mchezo wa kesho dhidi ya Prisons kuwa ni kama alizotumia katika mchezo dhidi ya Mbeya City Jumatano wiki hii.

Katika mechi hiyo, Sven alitumia mipira ya juu kutokana na Uwanja wa Sokoine kutoruhusu soka la pasi fupi ambalo tumelizoea kutokana na eneo lake la kuchezea (pitch) kutokuwa zuri.

Sven Vandebroeck

“Tutatumia mipira mirefu kama tulivyofanya katika mchezo uliopita dhidi ya Mbeya City, hatutacheza soka la pasi za chini kama kawaida yetu kwa kuwa hali ya uwanja haituruhusu kufanya hivyo,” Kocha Sven amefichua hayo alipokua akiongea na tovuti rasmi ya klabu ya  Simba.

Simba na utamaduni na kusifika kwa soka safi la pasi za haraka za chini lakini Kocha Sven ameamua kubadili mfumo huo ili kuendana na hali ya Uwanja wa Sokoine. Licha ya kuweka wazi kuwa atatumia mfumo wa mipira mirefu kocha Sven ameahidi kucheza soka safi la kuvutia kama ambavyo mashabiki wa soka wanavyopenda.

Jonas Gerad Mkude

Kuhusu hali ya kikosi kocha Sven amesema wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri na wapo tayari kwa mchezo isipokuwa kiungo Jonas Mkude ambaye anamalizia adhabu yake ya kufungiwa mechi mbili.

“Wachezaji wote wako vizuri wana ari tayari kwa mchezo wa kesho, isipokuwa tutaendelea kumkosa Mkude ambaye anamalizia adhabu yake ya kukosa mechi mbili,” amesema kocha Sven ambae anakaribia kuwa miongoni mwa makocha walioipa ubingwa klabu ya Simba!


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.