Tetesi

Manara ataja timu atakayokwenda Morrison.

Sambaza....

Baada ya klabu ya Simba kutoa taarifa rasmi kwa umma kuhusu hatma ya kiungo wao mshambuliaji Benard Morrison msemaji wa klabu ya Yanga amemtakia kila lakheri nyota huyo kutoka Ghana.

Haji Manara msemaji wa klabu ya Yanga amemtakia kila lakheri lakini pia akisema anajua Morrison anakwenda klabu kubwa ndani ya Bara la Afrika.

Benard Morison “shibobo style”

“Kila lakheri huko uendako, kwa taarifa nilizozipata mida hii najulishwa unaelekea klabu kubwa Barani Afrika.” Haji Manara

Anaandika Haji katika ukurasa wake wa instagram “Sijajua ni timu gani ila najua ni klabu kisawasawa ndani ya Bara hili kubwa. “Lecturer” inshaalah utapata “university” yakweli muda si mrefu,”

Benard Morrison akishangilia goli na John Bocco katika mchezo dhidi ya US Gendamarien

Benard Morrison alijiunga na Simba misimu miwili iliyopita akiyokea Yanga na kufanikiwa kutwaa Kombe la FA na ubingwa wa Ligi Kuu Bara akiwa na Simba.

YouTube player

Sambaza....