Sambaza....

Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya soka ya Simba ya jijini Dar es Salaam, Haji Sunday Manara amewajia juu watu wanaosambaza ujumbe kwenye mitandao ya Kijamii kuwa amefungiwa na shirikisho la soka nchini TFF.

Manara amesema watu wa namna hiyo ni wale ambao kwa namba moja ama nyingine wanamchukua yeye na klabu ya Simba kwani sababu ambayo wanaitaja ya kufungiwa kwake haina mashiko yoyote.

Amesema hata kama watu hao wataendelea kusambaza hila dhidi yake lakini yeye bado anaaminika na uongozi wa juu wa klabu na kwanza ataondoka pindi muda wake utakapoisha na wala haipaswi kusambazwa kwa jumbe za kumkorofisha yeye na viongozi wake.

“Kinachosambazwa kwenye mitandao na magroup ya WhatsApp kupitia audio clip eti nimesimamishwa na TFF ni upuuzi..ni wale wale ambao ama wanaichukia Simba au wanamchukia Haji binafsi..sijawahi na sitawahi kushawishi Wanasimba wavamie jengo la Yanga, kama inavyosema hiyo clip..najua kuna watu wanaumia sana uwepo wangu pale..ila niwahakikishie Bodi nzima ya Wakurugenzi chini ya Mwenyekiti wake Bw Mohammed Dewji MO inanipa full support,Wanachama na washabiki wetu halikadhalika…So puuzeni matango pori ambayo yamemnukuu Rais wa TFF ambao so far tunafanya kazi nao vema…Governor yupo sana kwenye mpira hadi Mungu atakapoamua vinginevyo”.

Aidha Simba itajitupa jioni ya leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam kucheza na African Lyon katika mfululizo wa mechi za ligi kuu soka Tanzania Bara.

Sambaza....