Ligi Kuu

Manara: Nitaachana na usemaji!

Sambaza....

Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amesema ikifika wakati ataachana na usemaji katika maswala ya soka ni kujikita katika mambo mengine.

Haji Manara ambae amevitumikia vilabu vyote viwili vikongwe vya Simba na Yanga katika idara hiyo na kuweka rekodi kua msemaji alietumikia pande zote mbili za klabu hizo za Kariakoo.

Haji Manara msemaji wa klabu ya Yanga

“Ikifika mwaka 2024 nitaachana na usemaji unajua nimekaa mdaa mrefu kwaiyo natakiwa nifanye mambo mengine. Tayari naanza kuandaa watu wengine ili kuchukua nafasi.” Alisema Haji Manara.

Manara amesema ataachaha na usemaji na kuhamia katika siasa huku akitanambaisha mpango wake wa kua mbunge.

“Nataka niachane na hii kazi ili nifanye mambo mengine, unajua naweza kuingia kwenye siasa nikawa mbumge labda.
Wakati ukifika ntaitisha “press” na ntaeleza kila kitu.” Haji Manara msemaji wa Yanga.

Sambaza....