Ligi KuuUhamisho

Mgosi ‘again’? Naweka karata yangu kwake

Sambaza....

MUSSA Hassan Mussa Mgosi amerudi tena uwanjani baada ya miezi kadhaa kujitokeza uwanja Taifa kulikokuwa kumetamalaki mashabiki wa Simba na kuchukua kipaza sauti na kusema ameamua kustahafu soka.

Japo nilikuwa mbali na Mgosi alipokuwa akizungumza maneno yale, lakini alionekana kama mtu aliyestahafishwa sio kustahafu kwa matakwa yake. Alitoa chozi la hisia, huku akiwa amembeba mwanae mmoja. Ilisisimua sana.

Hivi sasa tutamuona tena Mgosi katika jezi za timu ya Dodoma Dfc inayonolewa na Jamhuri Kihwelo Julio Alberto. Mgosi na Julio ni kama mtu na baba yake, rafiki yake, mwisho kabisa wanabaki kuwa kocha na mchezaji wake.

Mgosi mchezaji. Julio kocha. Hapa kutakuwa na ahadi ya nyuma ya pazia ambayo mimi na wewe hatuijui. Anayeijua ni Julio na Mgosi.

Julio kocha mshindani. Hawezi kuingia sokoni tena kwenye dirisha dogo kama hili akamsajili mchezaji wa hovyo. Naamini kuna mabao ya mwisho mwisho ambayo Mgosi hakuyafunga ataenda kuyafunga wakati huu.

Katika usajili huu wa Mgosi, nasimama na Julio. Mgosi anaufahamu vyema mpira wa Tanzania kama ilivyo Okwi. Anavifahamu viwanja vingi, unadhani anaenda kubadili mitindo ya nywele kama wanavyobadili rafiki zangu wengi? Ninaposema kuna ahadi kati ya Julio na Mgosi, napaswa kueleweka si vinginenyo.

Mpira wa Tanzania ni rahisi sana. Wachezaji wanacheza hawako fiti. Wachezaji wanacheza kijanja sana kwa kujijengea vieneo uwanjani, katika misingi hii unadhani Mgosi ataenda kushindwa tena kwenye ligi ya daraja la kwanza inayotumia nguvu kuliko akili?

Ningejawa mashaka na hofu kama Mgosi angeenda kucheza nje ya nchi. Huko nje watu wanafanya sana mazoezi, wanapumzika kwa wakati, huko kungeweza kumshinda Mgosi, lakini hapa ndani katika ligi ambayo wachezaji wake wanatumika sana nje ya uwanja kuliko nje, naweka karata yangu kwa Mgosi.

Umri ni namba. Kinachomata ni ubora wa mchezaji. Siamini kama Julio amemsainisha Mgosi kwa ajili ya kwenda kumbebea dawa za kuleta ushindi, amemsainisha baada ya kuona kazi inayopaswa kufanywa na vijana wengi ikiwashinda. Amekwenda kwa kazi maalum.

Aliwahi kushangaza mwandishi mmoja wa Zimbabwe aliyekuja nchini kutazama maendeleo ya Wazimbambwe wenzake Thaban Skalah Kamusoko na Donald Dombo Ngoma. Jamaa yule alishangaa na kusema mbona hawa wachezaji wanacheza kawaida? Umegundua kitu gani hapa? Ngoma, Kamusoko wanacheza ligi dhaifu yenye wachezaji dhaifu. Hapa kwa vyovyote vile, wao wataonekana bora kushinda wenzao wasiokuwa bora.

Nasimama na Mgosi. Hapa naona Julio kafanya moja ya sajili bora ya kuisaidia Dodoma FC. Mwanjali mwenyewe kaondolewa Simba kutokana na majeruhi, sio ubora. Lakini katika ligi za kishindani ni ngumu kumuona Mwanjali akitamba na kupata sifa kama alizopata nchini. Lakini kwa Tanzania alionekana beki aliyeshindikana kupitika.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x