Jonas Gerad Mkude
Ligi Kuu

Mkude mechi imemshinda, kocha amkomalia Chama!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Simba jana imecheza michezo miwili ya kirafiki katika uwanja wake uliopo Bunju jijini Dar es salaam na kuweza kuibuka na ushindi katika michezo hiyo yote. Simba ilicheza asubuhi dhidi ya Transit Camp na jioni dhidi ya KMC.

Katika mchezo wa asubuhi Simba ilicheza na Transit Camp na kuifunga mabao manne kwa mawili, huku jioni pia wakiifunga KMC mabao matatu kwa moja.

Jonas Gerald Mkude akimuacha mchezaji wa FC Leopard

Katika mchezo waliocheza jioni dhidi ya KMC kiungo Jonas Mkude alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kupata majeraha mwanzoni mwa kipindi cha pili. Jonas aligongana na mshambuliaji Serge Tarpei wa KMC na kumfanya kushindwa kuendelea kucheza na kupelekea kuondolewa uwanjani hapo na gari la wagonjwa.

Baada ya Jonas Mkude kuumia na kutoka nje nafasi yake ilichukuliwa na Ibrahim Ajib Migomba. Bado taarifa rasmi ya klabu haijatoka kiungo huyo atakaa nje kwa muda gani.

Clatous Chama

Kwa upande mwingine tovuti yako pendwa ya Kandanda ilikiwepo uwanjani hapo na kumshuhudia kiungo Clatous Chama akiwa kwenye mazoezi katika uwanja mwingine wa nyasi bandia pindi ambapo mchezo wa Simba na KMC ukiwa unaendelea.

Clatous Chama alikua na Miraj Athumani wakifanya mazoezi wakiwa chini ya usimamizi wa kocha wa viungo wa Simba Adel Zrane. Kocha huyo wa viungo alionekana akiwapa mazoezi ya mpira na koni.

Adel Zrane alipanga koni uwanja mzima huku akiwataka wachezaji hao wawili wachezee mpira huku pia wakipitia katika koni hizo zilizojaa uwanja mzima. Miraj Athumani na Clatous Chama walifanya mazoezi hayo kwa dakika 90 mpaka pale mchezo ulipomalizika wa Simba na KMC.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.