
Feisal Salum akisalimiana na Jonas Mkude katika mchezo dhidi ya Simba
Kuelekea mchezo wa robo fainali wa kombe la FA kati ya Azam fc na Simba sc, klabu ya Simba imepata nafuu katika eneo la kiungo baada ya Jonas Mkude kumaliza adhabi yake na kupona majeraha aliyoyapata katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMC.
Lakini pia kocha mkuu wa Simba Sven ameongeza kuwa mchezo wa leo utakuwa mgumu kutokana na ubora wa wapinzani wao lakini yeye na benchi lake la ufundi wamekiandaa kikosi kwa ajili ya ushindi na ana matumaini ya kuhakikisha Simba inavuka kwenda nusu fainali ambapo itakutana na Watani zao Yanga sc.

Sven “Wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunajua Azam ni timu imara, ingawa tumeifunga katika mechi tatu zote zilizopita lakini bado haitufanyi tujisikie itakuwa rahisi tumejipanga kuhakikisha tunashinda.”
Pia kiungo Jonas Mkude amemaliza adhabu yake ya kutumikia mechi mbili alizokuwa amefungiwa na atakuwa huru kucheza kama benchi la ufundi litaona inafaa.
Kocha Sven amekuwa akiwatumia Said Ndemla, Gerson Fraga na Mzamiru Yassin katika eneo analocheza Mkude ingawa kwenye mechi ya leo huenda akaanzishwa.

Mshindi wa mchezo wa leo atakwenda kukutana na Yanga sc ambao jana walifanikiwa kuwafunga Kagera Sugar katika mchezo wa robo fainali uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini la Dar es salaam.
Unaweza soma hizi pia..
Alli Kamwe: Lengo Yanga na sio Mayele!
Mayele ni mchezaji muhimu kwenye Timu. Yanga inamuhitaji zaidi akiwa Fiti uwanjani kuliko yeye anavyokihitaji kiatu cha Ufungaji bora kabatini kwake.
Msemaji Simba: Mambo ni magumu!
Kila mwanasimba anatakiwa kufahamu hilo na kukubali mambo ni magumu.
Kola na mfupa uliomshinda Mayele!
Licha ya Fiston Mayele kusifiwa na kuoneoana ni moja ya washambuliaji hatari katika Ligi lakini hakufanikiwa kufunga
Alli Kamwe: Kumbe bila moto wanateseka!
: Asante Moalin. Asante Pablo Franco, Mechi ilichezwa sana kwenye mbinu kisha ikamalizikia kwenye Ufundi wa wachezaji.