Uhamisho

Mshambulaliaji wa Uganda kutimkia Villareal.

Sambaza....

Mshambuliaji chipukizi wa timu ya Taifa ya Uganda na Klabu ya Proline Fc amepata nafasi ya kwenda kufanya majaribio nchini Hispania katika timu ya Villareal baada ya kufanya vizuri katika michezo ya Kimataifa akiwa na Proline fc na timu ya Taifa ya Uganda.

Ivan Bogere anakwenda kufanya majaribio nchini Hispania ambapo kila kitu kimeshaandaliwa na sasa anasubiri tu mipaka ifunguliwe ili aweze kwenda nchini humo katika klabu hiyo ya Nyambizi wa manjano.

Ivan Bogere akiwaacha walinzi wa Tanzania katika michuano ya vijana ya chini ya umri wa miaka 20.

Katika msimu huu pekee Bogere amefanikiwa kufunga mabao matano katika michezo minne ya CAF Conferederation Cup  akiwa na Proline Fc huku pia akiwa mshambuliaji kiongozi katika timu ya vijana ya Uganda ya U-20 The Hippos.

Ivan Bogere ni miongoni mwa nyota walioisadia Proline kupanda Ligi Kuu katika msimu uliopita baada ya kufanikiwa kufunga mabao 15 katika Ligi daraja la kwanza.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.