Ndemla na John Bocco
Mashindano

Namungo watatupa changamoto- Bocco

Sambaza....

Nahodha wa klabu ya soka ya Simba John Bocco “Adebayor” ametema cheche kuelekea mchezo wa Ngao ya Jamii na kujinasibu lazima waibuke na ushindi mbele ya Namungo.

Bocco “Tunaamini Namungo ni timu nzuri na itatupa changamoto, lakini tunaamini benchi letu, wachezaji tulionao kwa mapenzi ya Mungu tunaamini kesho tutafanya vizuri.”

Kocha mkuu wa Simba Sven Vandebroek pia ameonyesha hamu ya kupata ushindi mbele ya Namungl ili kuanza Ligi na morali lakini pia akisema wachezaji wake wapo tayari kwa mchezo.

Benard Morrison akishangilia goli lake la kwanza akiwa na jezi ya Simba, pamoja na kiungo Said Ndemla

Sven ” Ni muhimu kuanza na ushindi sababu itatupa nguvu ya kuanza Ligi vizuri wiki ijayo. Tutafanya kila jitihada kuhakikisha tunashida. Wachezaji 20 wapo tayari kwa mchezo.”

Namungo na Simba wanakwenda kukutana katika mchezo wa Ngao ya Jamii katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha siku ya Jumapili August 30.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.