Tetesi

Namungo yavamia tena Lipuli!

Sambaza....

Klabu ya soka ya Namungo fc imeendelea kujiimarisha kuelekea msimu ujao katika kipindi hiki cha usajili kwa kuwasajili nyota wa kusuka kikosi chao cha kushiriki Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.

Namungo fc wakati wowote kuanzia sasa huenda ikamtambulisha Paul Nonga “Baba Jackiee” ama Baba Paroko kama mchezaji wao mpya kwenda kuongeza nguvu katika eneo la ushambuliaji la vijana wa Lindi.

Nonga ambae hakumaliza msimu vizuri na klabu yale ya Lipuli baada ya kutofautiana na uongozi na hivyo kupelekea kushindwa kujiunga na timu kumalizia Ligi baada ya mapumziko ya ugonjwa wa corona kumalizika.

Lipuli iliyoshuka daraja tayari imemalizana na Nonga kutokana na mkataba kati yake na Nonga kumalizika msimu huu. Nonga anakwenda kuziba nafasi ya Reliant Lusajo ambae mpaka sasa hajasaini mkataba mpya.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.