Sambaza....

Ni kama michezo ya kufuzu Afcon nchini Cameron imekuja na neema kwa wachezaji wawili wa Simba baada ya kocha Mfaransa kuwahitaji kikosini kiungo Haruna Niyonzima wa Rwanda na beki Juuko Mursheed wa Uganda.

Wachezaji  hao wawili wa Kimataifa  wametakiwa na mwalimu Patrick Aussems baada ya kuonyesha viwango vizuri walipokua wanazitumikia timu zao za Taifa katika kufuzu Afcon 2019 Cameroon. Huku Haruna Niyonzima akiitumikia Rwanda waliopoteza mbele ya Ivory Coast na Uganda wakitoka suluhu nyumbani na Tanzania.

Mwalimu Patrick alionyeshwa kuvutiwa na uwezo wa beki Juuko Mursheed alieweza kumdhibiti vilivyo Mbwana Sammata na kusema ana sifa zote za kua mlinzi katika michezo ya Kimataifa. Katika mchezo uliofanyika katika dimba la Nambolee jijini Kampala Juuko Mursheed aliweza kuwadhibiti washambuliaji wa Taifa Stars wanaocheza soka la kulipwa wakiongozwa na Simon Msuva wa El Jadida, Mbwana Sammata wa Krc Genk na Thomas Ulimwengu wa Al hilal.

Wachezaji wote wawili tayari wapo jijini Dar es salaam wakimalizana na uongozi wa klabu chini ya Kaimu raisi “Try again” ili kuweza kuungana na wenzao waliopo kambinii. Wachezaji hao huenda wakaungana na wenzao watakaobaki jijini Dar és salaam na kocha msaidizi Masoud Djuma kuendelea kujiweka sawa baada wachezaji 20 na kocha mkuu wa Simba kuelekea Mtwara kucheza na Ndanda fc.

 

Sambaza....