Uhamisho

Nonga apiga U-Turn kali

Sambaza....

Licha ya kushuka Daraja, Lipuli Fc yenye makazi yake mjini Iringa, wachezaji wake wameendelea kupata usajili katika vilabu vingine.

Mtandao wetu umepata taarifa za uhakika kuwa aliyekuwa Mshambuliaji na Nahodha wa Lipuli FC, Paul Nonga, sasa amejiunga na Gwambina Fc baadala ya Namungo Fc kama tulivyoripoti awali.

Paul Nonga (Julia)

Nonga anaelekea katika timu hii ya Gwambina kuungana na Papa Mwinyi Zahera ambaye ni mkurugenzi was ufundi wa timu hiyo.

 

Huyu ni mshambuliaji makini na hatari, akiwa amefunga mabao 10 katika msimu uliopita wakati akiwa na Lipuli FC, Amewahi vichezea vilabu vya Yanga na Mwadui pia.

Sambaza....