AFCON

Okwi hakustahili kupata dakika nyingi dhidi ya Stars

Sambaza....

Uganda “The Cranes” walipata kipigo kingine tena katika mechi ya kufuzu Afcon 2023 bao likifungwa na Simon Msuva kipindi cha pili wakati Tanzania ilipoibuka na ushindi wa bao 1-0 nchini Misri.

Vijana wa Micho sasa wako mkiani mwa Kundi F wakiwa na pointi moja kutoka kwa pointi tisa baada ya michezo mitatu. Hivi ndivyo kila mchezaji  alivyokadiriwa jioni ya jana baada ya kiwango cha kutatanisha huko Ismailia.

Jamal Salim Magoola – 5: Alibahatika kutoruhusu mpira wa adhabu uliopigwa na Novatus kipindi cha kwanza na akaokoa vyema na kuinyima bao Taifa Stars kipindi cha pili kabla ya kufungwa bao la kufutia kutoka kwa Msuva.

Kenneth Ssemakula – 4: Alicheza nje ya nafasi aliyokuwa akiipenda lakini hakuonekana kuwa na nafasi ingawa alijaribiwa sana Msuva na Samatta waliposhambulia hasa kipindi cha kwanza.

Azizi Kayondo – 5: Alikuwa na wakati mzuri kipindi  cha kwanza lakini hakua katika eneo sahihi wakati Muzamir Yassin anapiga pasi  kumpatia mpira Dickson Job ambaye krosi yake ya chini ilizaa bao la ushindi.

Livingstone Mulondo – 4: Alianza kwakushangaza mbele ya Timothy Awany na kupewa mtihani mzito na washambuliaji wa Taifa Stars hasa baada ya mapumziko waliporejea kipindi cha pili.

Nahodha na mshambuliaji wa Taifa Stars akitafuta njia mbele ya mlinzi wa Uganda.

Halid Lwaliwa -3: Hakutazama sehemu sahihi katika muda wote wa mchezo kwani mara kwa mara alikuwa akimiliki mpira na uongozi wake wa ulinzi haukuonekana kamwe.

Siraje Sentamu -5: Alitolewa wakati wa mapumziko licha ya uchezaji wa uhakika dhidi ya safu ya kati ya Taifa Stars iliyosheheni viungo.

Khalid Aucho -4: Mara nyingi alikuwa akikimbia na mpira katikati ya uwanja na kupelekea kuzuiliwa na wachezaji wa Stars kila mara na pasi yake ya kizembe ilikaribia kuipa Stars bao la pili.

Farouk Miya -1: Hakusahaulika kwa muda wote aliokuwa uwanjani na Stars. Alistahili kufanyiwa mabadiliko wakati wa mapumziko.

Emmanuel Okwi -2: Alidhibitiwa na kiungo wa kati mwenye umri wa miaka 20 ambae alicheza kama beki wa kushoto Novatus Dismass. Alipata dakika zaidi ya alizostahili, alipaswa kutolewa mapema.

Joseph Ochaya -3: Alikosa nafasi nzuri zaidi ya Uganda Cranes katika kipindi cha kwanza na hakuwa na marejeo mazuri aliyotarajia katika jezi za timu ya Taifa.

Fahad Bayo -4: Alifanyiwa mabadiliko kwa njia ya kushangaza wakati wa mapumziko licha ya nguvu na kasi yake katika ushambuliaji. Alipoteza mapambano na Ibrahim Baca mara nyingi sana.

Walioingia: Rogers Mato 2, Allan Okello 2, Ismail Mugulusi 6, Richard Basangwe 2.

Sasa Uganda watapaswa kwenda ugenini katika uwanja wa nyumbani wa Stars Benjamin Mkapa Machi 28 katika mchezo wa marudiano wa Kundi F.

Chanzo Kawowo Sports.


Sambaza....