EPL

Ole: Mpeni muda Sanchez.

Sambaza kwa marafiki....

Kocha wa muda wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amesema anaamini kiwango cha mshambuliaji wake Alexis Sanchez kitaimarika licha ya kutupiwa lawama na mashabiki wake kutokana na kucheza chini ya matarajio ya wengi.

Sanchez ambaye ni raia wa Chile alisajiliwa na Manchester United katika dirisha dogo la usajili mwaka jana lakini toka kipindi hicho amefanikiwa kufunga mabao matano pekee na licha ya kuwa chini ya kiwango lakini pia amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara.

“Tunajua kuna mchezaji mzuri sana ndani ya Sanchez, ni kama chupa yenye gesi, ikiamua kutoka inatoka na ninaimani atakuja kuwa mchezaji mzuri,” Solskjaer amesema.

Manchester United wanajiandaa kucheza na Chelsea leo jumatatu katika mchezo wa kombe la Chama cha soka England kwenye uwanja wa Stanford Bridge na Sanchez anatarajiwa kuwa miongoni mwa nyota watakaocheza kutokana na Winga Antony Martial kuumia.

“Kila mtu anatamani kucheza fainali ya FA Cup, kwangu mimi ni kumbukumbu kubwa sana hasa tulipocheza dhidi ya Newcastle United, kwa sasa Tunakataka kujaribu FA Cup na ndio tunaagalia namna ya kuweza kutwaa taji hilo,” Soleskjaer amesema.

Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.