Uhamisho

Samata rasmi EPL, atambulishwa Villa kwa kiswahili!

Sambaza....

Baada ya kusubiri kwa hamu tetesi za Mbwana Samata kujiunga na klabu ya Aston Villa sasa imekua si tetesi tena bali ni kweli baada ya klabu hiyo kumtambulisha rasmi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii.

Mbwana Samata ahamisho wake ni kama ulikua unachelewa hivi na hii ni kutokana na maswala ya  kupata vibali vya kufanyika kazi katika nchi ya Uingereza.

Mbwana Samata amesaini kandarasi ya miaka minne na nusu huku akisajiliwa kwa kiasi cha pauni milioni kumi kutoka klabu ya KRC Genk ya nchini Ubeligiji.

Mbwana Samata

Katika ukurasa rasmi wa Aston Villa klabu hiyo imemtambulisha Mbwana Samata kwa kuandika “New Signing, Karibu Sana Mbwana Samata”

Samata mchezaji wa zamani wa African Lyon, Simba sc na TP Mazembe anakua Mtanzania wakwanza kucheza katika Ligii Kuu nchini Uingereza maarufu kama EPL.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.