Thadeo Lwanga akifunga bao mbele ya walinzi wa Yanga katika fainali ya Kombe la FA Kigoma katika uwanja wa Lake Tanganyika
ASFC

Simba na Yanga kukutana tena mwezi huu.

Sambaza....

Ratiba ya kombe la Azamsports Federation Cup imetolewa leo na Shirikisho la Soka nchini TFF huku pia wakitaja na viwanja vitakavyotumika katika michezo hiyo ya nusu fainali.

Nusu fainali ya kwanza itawakutanisha Yanga na Simba katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza May 28. Simba waliitoa Pamba fc wakati Yanga waliitoa Geita Gold katika michezo ya robo fainali.

Ratiba ya nusu fainali ya kombe la FA.

Nusu fainali ya pili itawakutanisha Azam Fc na Coastal Union katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid May 27 mkoani Arusha.

Simba na Yanga watakua wanakutana mara ya pili mfululizo katika michuano hiyo ambapo mara zote Simba ameibuka kinara. Simba na Yanga walikutana katika mchezo wa fainali ya FA msimu wa 2020/2021 na Simba kuibuka na ushindi wa bao moja bila. Katika msimu wa 2019/2020 pia walikutana nusu fainali na Simba kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa moja katika Uwanja wa Taifa.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.