Uhamisho

Simba yaanza vurugu za usajili,yamshusha mmbaya wao!

Sambaza....

Klabu ya Simba sasa imeanza balaa katika usajili wa dirisha dogo baada ya kukaa kimya kwa muda huku wenzao Yanga wakitamba kwa kushusha vifaa vya maana.

Simba imeanza kujibu mapigo na sasa imeanza na winga machachari aliyewafunga katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Africa na kuwafanya kutolewa mapema katika michuano hiyo.

Luis Misuiquone akikaribishwa na kocha mkuu wa Simba sc Sven Van De Broek!

Luis Misuiquone ametambulishwa rasmi leo na Simba akitokea klabu ya Mamelody Sundowns ambao walimtoa kwa mkopo katika klabu ya UD Songo ya nchini Msumbiji.

Luia ametambulishwa leo na kocha mkuu wa Simba Sven Vandebroek huku akionekana mwenye furaha na shauku ya kuitumikia Simba.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.