Uhamisho

Siondoki Yanga -Tshishimbi

Sambaza....

Kuna hadithi mbili mpaka sasa hivi ambazo hazieleweki kwenye klabu ya Yanga. Hadithi ya kwanza ni ya Yanga na Bernard Morrison.  Kila upande wa hadithi hii unadai hauna makosa kwenye changamoto wanazopitia.

Yanga wanadai wako na mkataba na Bernard Morrison unaoisha mwaka 2022 wakati Bernard Morrison anadai mkataba alionao unaisha mwezi huu. Kitu ambacho kinawaacha wengi njia panda kwa kutotambua kipi ni sahihi.

Papy

Hadithi ya pili ni ya Yanga na Papy Kabamba Tshishimbi , wengi hawajui hatima ya Yanga na Papy Kabamba Tshishimbi. Hawana uhakika kama Papy kabamba Tshishimbi katia saini. Lakini jana kwenye maonesho ya sababa Tshishimbi alidhibitisha kubaki Yanga.

“Bado niko yanga bado niko yanga, Tulisha fanya mazungumzo na uongozi wa klabu kuhusu kusaini mkataba mpya baada ya siku mbili hizi tutamalizana.”alisema Papy Kabamba Tshishimbi.

Sambaza....