Mashindano

Stars yafia kwa mwenyeji!

Sambaza....

Safari ya Kilimanjaro stars imefikia tamati leo katika mchezo wa nusu fainali baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya timu mwenyeji wa mashindano hayo.

Stars imekubali kichapo cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Uganda na hivyo kupoteza nafasi ya kufuzu fainali na kuwaacha wenyeji Uganda kusonga mbele na kucheza na Eritrea katika fainali.

Kwa matokeo hayo sasa ni timu za Kundi A Eritrea na Uganda ndio zitakazomenyana fainali na kuweza kumpata mshindi wa michuano  hiyo kwa mwaka huu.

Kilimanjaro itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kucheza vizuri na kuweza kuwazuia vizuri Uganda kabla ya  kuruhusu bao katika dakika ya 88 ya mchezo huo. Sasa Killi Stars inajiandaa kucheza na Kenya  kusaka mshindi wa tatu siku ya tarehe 19.

Kenya wao wamepoteza mchezo wa nusu fainali mwa mabao manne kwa moja dhidi ya Eritrea katika mchezo wa awali.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.