Wachezaji wa Simba wakiwa wamewasili Songwe Internationa Airport.
Ligi Kuu

Wachezaji wa Simba na kocha wao waachwa Dar

Sambaza....

Kikosi cha Simba tayari kipo jijini Mbeya tayari kabisa kwa mchezo dhidi ya Ihefu inayotokea maeneo ya Mbarali iliyopanda daraja msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Baada ya kumalizika kwa mchezo wa Ngao ya Jamii jijini Arusha kikosi chote cha Simba kilipanda ndege  kurudi Dar halafu wakaunganisha ndege kwenda Mbeya ili kuiwahi Ihefu.

Lakini timu ilipofika Dar baadhi ya wachezaji walibakishwa kutokana na maelekezo ya kocha mkuu Sven. Miongoni mwa wachezaji waliobaki Dar ni pamoja na Lusi Miquissone, Pascal Wawa, Cris Mugalu na Ally Salim. Lakini pia kocha wa viungo Adel Zrane pia alibaki Dar.

Sababu kubwa ya wachezaji hao kubaki Dar na kutokuambatana na timu Mbeya ni kukosa utimamu wa mwili kuelekea kuanza kwa Ligi. Pascal Wawa na Luis wao baada ya Ligi kuisha walipewa ruhusa yakwenda kufunga ndoa, lakini pia Mugalu inaelezwa alirudi kwao Congo.

Wachezaji hao watatu tangu jana asubuhi wameonekana katika viwanja vya Simba Bunju pamoja na mwalimu wa viungo Adel Zrane akiwasimamia kufanya mazoezi ya nguvu na ya mpira ili kurudisha utimamu wa mwili.

 


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.