Kibwana Shomari
Uhamisho

Yanga wameiba mchezaji wetu-MTIBWA

Sambaza....

Suala kubwa kwa sasa kwenye anga la mpira wetu ni suala la Bernard Morrison na klabu yake ya Yanga. Yanga wanadai kuwa wana mkataba na Bernard Morrison mpaka 2022 na Bernard Morrison amedai hana mkataba na Yanga.

Wakati hili na Bernard Morrison halijaisha limeibuka jingine ambalo ni la Kibwana Shomari ambaye ni mchezaji mpya wa Yanga ambaye amesajiliwa kutoka Mtibwa Sugar.

Akizungumza na tovuti hii , Afisa Habari wa klabu ya Mtibwa Sugar , Thobias Kifaru amedai kuwa Kibwana Shomari ana mkataba na klabu ya Mtibwa Sugar na Yanga wamemnunua bila kuwasiliana na Mtibwa Sugar.

“Kibwana Shomari ana mkataba na Mtibwa Sugar. Najua Kibwana Shomari ni kijana mdogo miaka 19 tu amerubuniwa na Yanga lakini ni mchezaji halali wa Mtibwa Sugar”- alisema Thobias Kifaru.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.