Ligi Kuu

Yanga yashindwa kuvunja gereza, Mayele aweka rekodi.

Sambaza....

Ligi Kuu Bara imeendelea leo kwa mchezo mmoja ambapo Yanga walikua wenyeji wa Tanzania Prisons katika mchezo wa raundi ya 23.

Yanga waliialika Tanzania Prisons katika dimba la  Benjamin Mkapa na mchezo huo kumalizika kwa sare ya bila mabao na kupelekea timu hizo kugawana alama moja moja.

Feisal Salum wa Yanga akitafuta mbinu za kumtoka mlinzi Vedastus Mwihambi wa Tanzania Prisons.

Licha ya kutengeneza nafasi nyingi za kufunga pamoja na kupata mkwaju wa penati lakini Yanga walishindwa kuzitumia na kupelekea sare hiyo na kuicha Prisons kuondoka na alama moja.

Yanga imeendeleza kudondosha alama katika NBC Premier League ambapo katika michezo yake mitatu ya mwisho wameambulia alama tatu baada ya michezo yote kutoka suluhu.

Fiston Kalala Mayele

Katika michezo yote hiyo mshambuliaji wa Yanga na kinara wa mabao katika NBC Premier League Fiston Mayele alikuepo uwanjani na hajafanikiwa kufunga goli hata moja hivyo kumfanya kuchezo michezo mingi zaidi mfululizo bila bao.

Licha ya kupata penati katika mchezo wa leo dhidi ya Prisons lakini alishindwa kukwamisha mpira wavuni baada ya penati yake kuota mbawa.

Kwa matokeo hayo Yanga inabaki kileleni wakiwa na alama 56, Tanzania Prisons wao wamepanda nafasi moja kutoka ya 15 mpaka ya 14 wakiwa na alama 23 wakimshusha Ruvu Shooting.

Sambaza....