George Mpole
Uhamisho

Yanga yamshindwa mshambuliaji wa Stars

Sambaza....

Klabu ya Yanga iliyokua inamfukuzia mshambuliaji wa timu ya Taifa na Geita Gold George Mpole ni kama imepigwa bao katika usajili huo baada ya mchezaji huyo kuwakacha na kusaini kwingine.

George Mpole tayari ameshasaini kuongeza mkataba wa mwaka mmoja wa kuendelea kuwatumikia waajiri wake wa sasa matajiri wa dhahabu Geita Gold.

George Mpole akimtoka mlinzi wa Simba Joash Onyango.

Akizungumza na kituo kimoja cha redio hapa nchini msemaji wa klabu ya Geita Gold Hemed Kivuyo amelithibitisha hilo.

“Baraza la michezo la manispaa na madiwani wote wa Geita walikaa chini na Mpole (George) na kukubaliana kuongeza mkataba wa mwaka mmoja ambao utamalizika mwishoni mwa mwezi ujao,” Hemed Kivuyo

“Kama kuna klabu yoyote inayoongea na Mpole kwasasa ili kutaka kumsajili  wanafanya makosa kisheria kwasababu Mpole ana mkataba nasi hivyo ni vyema wakaacha mara moja. Kusaini kwake Geita haiimaanishi hawezi kuondoka lakini waje mezani tuzungumze sio kuishia tuu mitandaoni kuonyesha wanamtaka mchezaji.,” aliongeza Kivuyo.

George Mpole akishangilia goli alilofunga na wachezaji wenzake wa Stars  katika mchezo dhidi ya Niger.

George Mpole alijiunga na Geita Gold akitokea Polisi Tanzania mpaka sasa ana mabao 14 akiwa kinara wa ufungaji wa mabao katika Ligi Kuu ya NBC pamoja na Fiston Mayele.

Kutokana na fomu yake nzuri msimu huu amekua akivivutia vilabu vikubwa nchini kutaka huduma yake huku Yanga ikitajwa zaidi kuhusishwa nae.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.