Uhamisho

Bwalya atambulishwa rasmi Afrika Kusini

Sambaza....

Kiungo fundi raia wa Zambia Rally Bwalya baada ya kuachana na Simba na kutimka nchini kuelekea Afrika Kusini leo ametambulishwa rasmi katika klabu yake mpya.

Bwalya alicheza mchezo wa mwisho wa Simba dhidi ya KMC ambao pia ulitumika kumuanga nyota huyo maarufu kwa jina la *Left footer magician”.

Rarry Bwalya.

Rally ametambulishwa rasmi na klabu ya Amazulu ya nchini Afrika Kusini hivyo msimu ujao atawatumikia Wazulu hao katika PSL Ligi Kuu ya nchini Afrika Kusini.

Bwalya alijiunga na Simba Agosti 2020 akitokea Power Dynamos ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu. Mpaka anaondoka Simba na kujiunga na Amazulu  alikua amesalia na mwaka mmoja. Inadaiwa amesaini miaka miwili kuwatumikia Amazulu.


Sambaza....
Tafadhali tumia viungo vya mitandao ya jamii kusambaza.