Uhamisho

Carlinho ana mkataba wa miaka 2 na Yanga

Sambaza....

Kulikuwa na uvumi kuwa mchezaji mpya wa Yanga kutoka Angola ana mkataba wa miezi sita na klabu ya Yanga. Kauli hii imekanushwa na injinia Hersi Said.

Injinia Hersi Said amedai kuwa Yanga na Carlinho wanamkataba wa miaka miwili mpaka sasa hivi na kama kutakuwa na uwezekano wa kuongeza wataongeza.

“Hizi ni taarifa ambazo zimekuwa zikitoka bila uthibitisho. Yanga na Carlhino wana mkataba wa miaka miwili. Ndani ya mkataba kuna kipengele cha kuongeza mkataba kama ataonesha kiwango kikubwa”- alidai Injinia Hersi Said.

Carlinhos Carmo

Injinia Hersi Said ametoa ushauri kwa baadhi ya waandishi wa habari ambao hutoa habari za uongo kujitazama mara mbili.

“Tunatoa wito kwa baadhi ya waandishi wa habari wanaotoa habari ambazo hazina ukweli wajiangalie mara mbili kwa sababu wanajiharibia wenyewe”- amedai Injinia Hersi Said.

Sambaza....