AFCON

Kapombe na Tshabalala wamerudi bwana

Sambaza....

Kile kilio cha wapenzi wengi wa Timu ya Taifa ya Tanzania “Taifa Stars” ya kutaka walinzi wa pembeni wa Simba Shomary Kapombe na Mohamed Hussein “Tshabalala” kujumuishwa timu ya Taifa hatimae kimesikika.

Rais wa TFF Wallace Karia amesema wawili hao tayari wapo kambini na wenzao wakijiandaa na mchezo wa marejeano dhidi ya Uganda katika mchezo utakaopigwa Machi 28 mwaka huu katika uwanja wa Benjamin Mkapa.

Shomary Kapombe

“Maneno yalikuwa mengi sana baada ya uteuzi uliofanyika mwanzoni lakini tumeona matunda yake, kuongezwa kwa Kapombe na ‘Tshabalala’ ni pendekezo la Kocha Mkuu, Adel Amroache na tayari wamejiunga kambini na wenzao,” alisema Wallace Karia.

Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Misri Taifa Stars iliibuka na ushindi wa bao  moja kwa sifuri, goli lililofungwa na Simon Msuva akiunganisha krosi ya Dickson Job.

Novatus Dismas

Walinzi hao wa pembeni wa Simba Shomary Kapombe na Mohamed Hussein katika mchezo wa kwanza nafasi zao zilizibwa na Dickson Job na Novatus Dismas ambao kiasili si walinzi wa pembeni licha ya kucheza vyema katika mchezo huo wa ugenini.


Sambaza....