Uhamisho

Kibwana: Inawauma lakini nipo Yanga!

Sambaza....

Mlinzi wa pembeni wa Yanga Kibwana Shomary ameongeza mkataba wa miaka miwili na Yanga na kuzima tetesi zote zakuondoka kwa Wananchi msimu ujao.

Kibwana alijiunga na Yanga misimu miwili iliyopita akitokea Mtibwa Sugar akiwa kama mlinzi wa kulia lakini ujio wa Djuma Shaban ulimfanya kuhamia kushoto na kuendelea kuonyesha kiwango bora. 

Kibwana Shomari (kulia) na Yassin Mustapha (kushoto) katika utambulisho wa wachezaji siku ya Wananchi.

Kulikuwepo na tetesi za Kibwana kuhitajika na Simba lakini Kibwana ameongeza miaka miwili na kuendelea kutumikia rangi za kijani na njano misimi miwili tena.

”Nipo ndani ya Yanga kwa sasa na hii ni habari nzuri kwa wengi ambao wanapenda mimi kuwa hapa kwa Wananchi kuendelea kufanya kazi,” alisema Kibwana

“Kwa wale ambao hawapendi nina amini kwamba itawauma basi wakae kimya na kwa sasa nipo ndani ya Yanga kama Wananchi wamenitaka mimi nani niweze kukataa kusaini Yanga?” Kibwana Shomary.

Uwepo wa Kibwana Shomary tena kwa miaka miwili Yanga kunahatarisha nafasi za walinzi wa kushoto wa Yanga pia kina Yassin Mustapha na Bryson Raphael. 

Sambaza....