John Bocco
Ligi Kuu

Kikosi bora cha ligi kuu Tanzania 2017/2018.

Sambaza....

1: Aishi Manula.


Golikipa bora wa Tanzania kwa misimu miwili iliyopita, kuilinda milingoti mitatu ya Azam Fc kulimpa nafasi ƴya kuonesha uwezo wake. Uwezo ambao haukuwa na shaka kwenye mboni za macho ya wengi.

Msimu huu analinda lango la msimbazi na katika mechi alizofanikiwa kucheza akiwa Simba amefanikiwa kupata clean sheets (19) mpaka sasa hivi na hii ni dalili tosha kuwa Golden Golves zinaenda kwake msimu huu pia na amegeuka kuwa mhimili mkubwa wa Simba mpaka sasa hivi.

2: Erasto Nyoni.


Mchezaji mwingine aliyesajiliwa kutoka Azam FC. Ameisaidia sana Simba msimu huu katika nyanja zifuatazo: Moja, amecheza nafasi nyingi ndani ya kikosi cha Simba ( beki namba mbili, beki wa kati na kiungo wa kuzuia). Pia amekuwa akihusika katika utengenezaji wa magoli pamoja na ufungaji wa magoli.

3: Asante Kwasi.


Beki mwenye uwezo utulivu mkubwa anapokuwa karibu na lango la mpinzani, mpaka sasa amefanikiwa kufunga magoli 8 kwenye ligi kuu , matano (5) akiwa Lipuli FC na magoli matatu (3) akiwa Simba. Na akiwa Simba amechezeshwa nafasi tatu kwa ufasaha mkubwa. Beki wa kati, beki wa kushoto na kiungo wa kati.

4: Kelvin Yondani.


Huyu ndiye mchezaji bora wa Yanga msimu huu. Kiwango chake kinaimarika kadri muda unavyozidi kwenda. Amekuwa beki bora kwenye majukumu ya kujilinda, uongozi na kuanzisha mashambulizi.

5: Yakubu Mohamed.


Moja ya usajili walionufaika nao Azam FC ni wa beki Yakubu Mohamed ni moja ya watu ambao wamekuwa mhimili mkubwa katika kikosi cha Azam FC, huyu ndiye mchezaji bora wa Azam FC kwa msimu huu mbele ya golikipa Razack Abarola.

6 : Jonas Mkude.


Hakuanza kucheza katika mzunguko wa kwanza , lakini alipopewa nafasi katika mzunguko wa pili alionesha thamani yake kubwa, thamani inayomfanya aingizie moja kwa moja kwenye kikosi hiki bora cha msimu huu.

7: Shiza Kichuya.


Mchezaji asiyeongelewa sana katika kikosi cha Simba, kwangu mimi huyu ndiye mchezaji bora wa Simba msimu huu. Amehusika katika magoli mengi msimu huu akiwa amefunga magoli saba na kutoa pasi za mwisho zaidi ya kumi na tano.

8: Mudathir Yahaya.


Singida United hawajajuta kwenye usajili huu. Amekuwa nguzo imara sana katika eneo la kiungo cha Singida Msimu huu.

9: John Bocco


Wakati anaondoka Azam Fc wengi tuliona kama kaisha na tulibeza uwezo wake lakini mpaka sasa hivi amefanikiwa kufunga magoli 14 na amegeuka kuwa nembo muhimu ndani ya kikosi cha Simba kama nadhodha.

10: Obrey Chirwa.


Moja ya nguzo imara ya safu ya ushambuliaji ya Yanga msimu huu baada ya wachezaji wengi wa safu hii kukosena msimu huu. Magoli 13 mpaka sasa hivi ashatupia kwenye ligi kuu.

11: Emmanuel Okwi.
Tulimwiita mhenga lakini mwisho wa siku katufanya tuone aibu na kejeli tulizokuwa tunamtolea. Mpaka sasa ana goli 20.


Kikosi hiki kutacheza mfumo wa 4-3-3.

Sambaza....
Subscribe
Notify of

0 Maoni
Inline Feedbacks
Tazama Maoni Yote
0
Tungependa kupata maoni yako, tafadhali tuambiax
()
x