Ndanda fc na Namungo walipokutana katika mchezo wakwanza wa Ligi
Ligi Kuu

Kiungo Namungo: Mechi ya Yanga ni muhimu kwetu!

Sambaza....

Kiungo wa zamani wa Simba na Friends Rangers ametoa onyo kwa Yanga huku akiwarangazia neema mashabiki wake na wa Namungo fc kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Yanga katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

John Mbisse ambae kwasasa yupo fiti  baada ya kupona vizuri kabisa majeraha ya kifundo cha mguu ambayo yalimfanya kukosa michezo mingi ya raundi ya kwanza ameitangazia vita Yanga katika mchezo wao wa Kesho alisema timu yake imejiandaa vizuri kwa mechi ya kesho na nyingine zote zilizobaki.

Kiungo John Mbisse akihamisha mpira mbele ya Abdalah Seseme wa Kagera sugar.

“Tumejiandaa vizuri kwa ajili ya mechi zote zilizobaki kwenye Ligi sio tu mechi ya Yanga, isipokuwa mechi na Yanga ni muhimu sana kwetu kutokana na nafasi na alama zetu kati yetu na wao. Mchezo utakua mgumu sana ila naimani alama tatu tutazipata katika mchezo wa kesho.” John Mbisse.

“Mashabiki zangu nawaomba waendelee kunisapoti nawaahidi sitowaangusha pindi ntakapopata nafasi katika mchezo wa kesho.” Alimalizia John Mbisse ambae ana uwezo wa kucheza kama kiungo wa ulinzi ama kiungo mshambuliaji.

Sambaza....